December 22, 2015

Screen Shot 2015-12-22 at 5.57.05 PM
Wakati Ujenzi wa Soko la Kimataifa Jijini Mwanza (Rock City Mall) ukiwa umeshakamilika, Kampuni za Kimataifa na Kitaifa zilizoanza kuwekeza ndani ya Jengo hilo, zimekumbushwa kuwapa kipaumbele cha ajira Watanzania, ili waweze kunufaika na uwekezaji huo.
Miongoni mwa wawekezaji waliowekeza ndani ya Jengo hilo ni Kampuni ya Vingíamuzi ya StarsTimes, ambayo imeanza kuajiri Vijana wengi, ikiwa ni moja kati ya mikakati yake inayolenga kuboresha huduma zake, lakini pia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Akielezea Mipango yao Meneja wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa Bakari Hassan, amesema wanatarajia kuuingiza mkoa wa Kigoma katika huduma zao, ili kuwawezesha wakazi wa mkoa huo kupata huduma ya Mawasiliano ya Luninga, sawa mikoa mingine hapa nchini.
Kutokana na mkakati huo mkuu wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Manju Msambya, amesema anamatarajio makubwa kuwa fursa za ajira zitafunguka pia mkoani Kigoma, huku akizihimiza Kampuni zinazowekeza ndani ya Soko la Rock City Mall kuiga mfano huo.
Wakati Kampuni hiyo ikiwa tayari imeshawekeza ndani ya Jengo hilo, Kampuni mbalimbali zinaendeleza kuwekeza, huku mamia ya vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini wakijitokeza kusaka ajira kutokana na uwekezaji huo

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE