December 30, 2015

 Msanii wa Nigeria anayetamba na kibao cha ‘Duro’, Tekno Miles anatarajia kutua jijini Dar es salaam wiki hii kwa ajili ya kufunga mwaka na fans wake wa Tanzania.

Msanii huyo ambaye wiki chache zilizopita ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Wash’, anatarajia kufanya show ya kufunga mwaka 2015, Dec, 31, kwenye ukumbi wa King Solomon jijini Dar.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Tekno anayedaiwa kuwahi kuwa na mahusiano na Agness Masogange ameonesha kujiweka karibu zaidi na mashabiki wa Tanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye baadhi ya post zake za kuhamasisha kuhusu show hiyo

Pia amerepost post ya muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael (Lulu).

 


Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE