Hospitali ya Temeke ya jijini Dar es salaam imekusanya zaidi ya Unit
100 za damu zilizotolewa na waumini wa dini ya Kiislamu kutoka Taasisi
ya Jamiiyat-Akhlaaqu- Islamiya wakiongozwa na viongozi wa halmashauri ya
Manispaa ya Temeke ili kukabiliana na Upungufu wa damu katika hospitali
hiyo.
Waumini hao wake kwa waume zaidi ya 150 walianza zoezi hilo la
kujitolea damu ikiwa ni muitikio wa kukabiliana na Upungufu wa damu
katika hospitali hiyo ambayo ilikuwa na Upungufu wa asilimia hamsini
kutokana na wagonjwa wengi kuhitaji huduma ya kuongezewa damu ikiwemo
akinamama wajawazito, watoto pamoja na majeruhi wa ajali.
Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya waumini waliojitolea damu wamesema
hatua hiyo inaonyesha uzalendo na kuwataka wananchi wengine kujitolea
damu ili kuwasaidia wananchi wengine wenye Shida
0 MAONI YAKO:
Post a Comment