January 27, 2016

Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania leo amelazimika kuahirisha Bunge kwa saa moja ili kamati ya uongozi ikae kujadili kauli iliyotolewa na Serikali kuhusu kisitishwa kwa matangazo ya bunge ya moja kwa moja yanayotolewa na Shirika la Habari la Taifa TBC.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kusema kuwa shirika hilo litasitisha kuonesha baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa lengo la kubana matumizi ya serikali katika uendeshaji wa shirika hilo.

Kauli hiyo ya waziri ilimfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kusimama na kutoa hoja ya kutaka bunge hilo liahirishwe ili kujadili suala hilo linaloashiria kuwanyima uhuru wananchi wakupata habari jambo lilizua mabishani bungeni humo.

Kutokana na shinikizo kutoka kwa wabunge wa upinzani kutaka bunge liahirishwe kwa ajili ya kujadili hoja hiyo Mwenyekiti wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge aliposema

Baada ya saa moja bunge lilirejea lakini likaahirishwa tena kutokana na kikao hicho kuwa hakijamalizika.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE