January 27, 2016

                           
Chelsea na West Brom watozwa faini

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu uwanjani katika mechi iliyozongwa na ubishi mwezi uliopita.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeitoza Chelsea faini ya pauni £65,000.

West Brom kwa upande wake imepigwa faiani ya pauni £35,000.

                      
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu

Mshambulizi mbishi wa Chelsea Diego Costa alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.

Mhispania huyo alishambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa.

West Brom walijifurukuta kutoka nyuma na kutoka sare na wenyeji wao Stamford Bridge.

                        
Costa alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari FA inasema kuwa timu zote mbili zilishindwa kudhibiti wachezaji wake.

Yacob, ambaye alikuwa keshaoneshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Costa, aliondolewa uwanjani na kocha Tony Pulis.

Siku chache baadaye kocha wa muda wa Chelsea Guus Hiddink alielezea kutoridhika na uamuzi wa refarii Anthony Taylor, akisema kuwa alipaswa kumuonesha kadi nyekundu Yacob

Related Posts:

  • Albamu mpya ya Barnaba kuandaliwa miezi mitatuMSANII wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’, amesema atatumia muda wa miezi mitatu kundaa albamu yake mpya. Akizungumza jijini hivi karibuni, Barnaba alisema matarajio yake ni kuingiza sokoni… Read More
  • Wanne wahukumiwa kifo MwanzaMahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Ge… Read More
  • Bajeti ya jeshi yaboreshwa China    China inasema kuwa bajeti yake ya ulinzi itaongezeka kwa asilimia kumi mwaka huu. Wanajeshi wake wanatarajiwa kupewa dola bilioni 145 na kuendelea na mfumo wa kuongeza bajeti ya jeshi ulioanza miaka 20 iliyo… Read More
  • Watu 35 wafa kwa mafuriko   Zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 55 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga  … Read More
  • Tanzania kukumbwa na ukame   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam.  Mamlaka ya Hali ya H… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE