Msanii Diamond Platnumz amekuwa akitajwa
mara nyingi kuwania tuzo mbalimbali na kusababishwa kuitwa jina la
‘Mond Bin Awards’, ametajwa kuwania tuzo za ‘MAYA’ (MOREKLUE ALL YOUTH
AWRDS 2016) za nchini Nigeria, ikiwa ndo nomination yake ya kufungulia
mwaka kwa mwaka huu 2016.
Ambapo Diamond anawania katika kipengele
cha ‘African Music Act’ akiwa pamoja na wasanii wengine wenye majina
makubwa Afrika akiwemo Wizkid, Sarkodie, Fuse ODG, Davido, AKA, Olamide
na Casper Nyovest.
Tuzo hizo za MAYA zitatolewa Januari 31, 2016 jijini Lagos, Nigeria.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment