January 17, 2016



Serikali imetoa siku saba kwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 baada ya kudaiwa kukiuka sheria za mazingira.
Baadhiya mambo yaliyobainika ni kukosa mfumo mzuri wa kuhifadhi na kusafirisha taka ngumu na taka maji, kutohifadhi vyema kemikali zinazotumiwa na kiwanda hicho pamoja na kutumia kuni kuendesha baadhi ya mitambo yake hususani eneo la kuchemshia.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanywa kwa ziara ya kushtukiza kiwandani hapo na naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Luhaga Mpina, aliyeambatana na wataalamu kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).
Mh Mpina amesema tayari serikali ilishakataza viwanda kutumia kuni na magogo kuendeshea mitambo yake, huku akitoa siku 30 kwa uongozi wa kiwanda hicho cha Mtibwa kufanyia marekebisho mapungufu yote yaliyotajwa vinginevyo serikali itakifungia.
Akiwa kiwandani hapo naibu waziri Mpina amewaagiza viongozi wa mamlaka mbalimbali kuwajibika katika agizo la usafi wa mazingira kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi sambamba na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuhakikisha miti milioni 1.5 inapandwa kila mwaka.
Kaimu meneja mkuu wa kiwanda cha sukari Mtibwa Ahmad Yahya pamoja na kuridhia maagizo yaliyotolewa, ameiomba serikali kuwapunguzia faini hiyo ya shilingi milioni 50 ambayo amedai kuwa ni nyingi kwa kiwanda hicho kumudu na kueleza namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika kiwandani hapo.


Related Posts:

  • Dayna Nyange na Nay kunani?? Picha zanaswa, wenyewe wakana Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi la nusu utupu na msanii wa Bongo Fleva, Aisha Nyange ‘Dayna’ Hii ni aibu yao! Picha zinazomuonesha staa wa Hip Hop anayetamba na ngoma ya Shika Adabu Yako, Emmanu… Read More
  • Wagombea warushiana matusi Marekani                      Wagombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Ted Crus na Donald Trump… Read More
  • Paul Makonda aombewa tena MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo. Zubery alimfanyia dua hiyo Makon… Read More
  • Wanajeshi 8 mbaroni kwa mauaji    Askari nane wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kigona wakituhumiwa kwa mauaji ya Erick Nilamewa (16) waliyemtuhumu kuwaibia simu moja aina ya Techno na Sh. 6,000. Tuki… Read More
  • Fatma Karume: Dk. Shein siyo rais Zanzibar Wakili Fatma Amani Abeid Karume MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani Fatma Amani… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE