Na Maafisa Afya na Mgambo wa halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam wamewatia mbaroni watu tisa baada ya kukaidi kushiriki zoezi la Usafi kwa kufungua maduka na kufanya biashara huku maeneo yanayowazunguka yakiwa machafu.
Kizaa zaa hicho kimewakumba wafanyabiashara hao katika eneo Mwembeyanga baada ya kufungua biashara zao, licha ya matangazo yaliyotolewa kwa wananchi kufunga biashara zao asubuhi na kushiriki usafi mpaka saa nne ndipo wafungue tena.
Kamata kamata hiyo pia iliwakumba vijana wanaouza maji katika mifuko ya plastik maarufu kama viroba ambayo serikali ya mkoa na manispaa ilipiga marufuku kwa kuwa sio safi na salama ambayo pia huchangia kuongezeka kwa ugonjwa wa kipindupindu…..
Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Wiliiam Mhemu amesema wananchi hao waliokamatwa wamekuwa wakikaidi amri ya kushiriki usafi kwa makusudi huku maeneo yao yakiwa machafu .
0 MAONI YAKO:
Post a Comment