February 24, 2016

                            
Ramo alikuwa na umri wa miaka 91

Ramon Castro, kakake mkubwa wa rais wa Cuba Raul Castro na aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Fidel Castro, amefariki dunia, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Ramon alikuwa na umri wa miaka 91.

Alikuwa mkulima na hakujihusisha na siasa ingawa alichangia sana katika sera za kilimo baada ya mapinduzi ya 1959.

"Asubuhi hii, mwenzetu Ramon Castro Ruz amefariki akiwa na umri wa miaka 91... maiti yake imechomwa na majivu yatarejeshwa eneo alikozaliwa,” mtangazaji wa tanzia yake alisema, bila kueleza sababu ya kifo chake.

Dadake, Angela, alifariki mjini Havana mwaka 2012.

                       
Ramon Castro alichangia sana katika sera za kilimo

Ramon Castro alizaliwa eneo la Biran, katika mkoa wa mashariki wa Holguin. Alikuwa wa pili kati ya ndugu saba wa mhamiaji Mhispania Angel Castro na mzaliwa wa Cuba Lina Ruz.

Nduguze walipojihusisha na vita na siasa, yeye alibaki akitunza shamba la familia.

“Mimi sijafanana na Fidel,” alizoea kusema kwa mzaha. “Yeye ndiye anayefanana nami, mimi ndiye mzee.”

                       

             Fidel Castro

Raul Castro, ndugu yao mdogo, alichukua majukumu ya uongozi kutoka kwa Fidel mwaka 2006 na akawa rasmi rais wa nchi hiyo 2008.

Raul Castro ana umri wa miaka 84 naye Fidel Castro miaka 89

Source: BBC

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE