Mwanamuziki Diamond asema alishangazwa na mapokezi aliyoyapata alipofika LodWar huko Kenya.
Wiki mbili zimepita tangu msanii Platnumz alipofanya show huko Kenya katika Club ya Marble na VIP Lounge. Ambapo show hiyo ilidhaminiwa na Club ya Marble, VIP Lounge na Mseto na kuweka historia kwa mapokezi ya nguvu.
Diamond aliulizwa na tovuti ya Mseto East Afrika kuhusu kitu kilichomshangaza na kumfurahisha alipofika LODWAR, alisema haya;
“Mapokezi ya airport, pia club tuliyoenda sikutegemea. Kabla sijaja niliambiwa ni jangwa kuna joto na mambo mengine. Nilijifunza vitu vingi sana”.
Diamond kwa sasa anatamba na kibao cha ‘Make Me Sing’ akiwa na msanii wa Afrika Kusini, AKA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment