February 15, 2016

                      
Hospitali ilivyo sambaratishwa

Makombora yameshambulia hospitali moja iliyoko upande wa kaskazini mwa Syria na kuua watu takribani kumi na saba.

Shirika la kujitolea misaada ya kitabibu la MSF, limesema kwamba hospitali hiyo iliyoko pembezoni yenye kutoa huduma katika jimbo la Idlib kwa hakika ilikuwa imelengwa kwa makusudi na shambulizi kutoka angani.

Mpaka sasa vifo vya watu saba vimethibitishwa kutokana na shambulio hilo, na watu wengine nane hawajulikani walipo. Hospitali nyingine katika mji huo nayo ilishambuliwa.

Mbali na tukio hilo, hospitali ya watoto imezingirwa na askari wa waasi wanaoshikilia mji wa Azaz ulioko karibu na mpaka na nchi ya Uturuki; katika mji wa Azaz imethibitishwa kwamba watu kumi wamepoteza maisha. Uturuki tayari imekwisha elekeza tuhuma zake kwa nchi ya Urusi kwa kuhusika na mashambulio yaliyotokea katika mji huo wa Azaz

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE