KUFELI AU KUFAULU…KWA MWANAFUNZI HAKUTOKANI NA UWEZO WA KIAKILI…
Tofauti kubwa kati ya mwanafunzi anaye faulu na anaye feli ni msukumo wa kusoma alio nao mwanafunzi husika, anaye faulu anakuwa na msukumo mkubwa wa kusoma ndani yake utakaompelekea kutumia nguvu kubwa kujifunza, na anaye feli anakuwa na msukumo mdogo, atatumia nguvu ndogo na focus ndogo.
JE huu msukumo hutoka wapi? kwa wazazi, walimu, ndugu, role models na kwenye jamii kwa ujumla.
Kama 76% ya wanafunzi wa liomaliza (form 4) wamefeli hii inamanisha msukumo wa kusoma ni mdogo less beauty(hauvutii) ukilinganisha na msukomo wa kutokusoma na mambo mengine ya kidunia yanayo chukuwa muda mwingi, akili na nguvu za wanafunzi.
Kwa nini msukumo wa kusoma ni.mdogo, na hauvutii (hauko sexy hautongozi hisia za wanafunzi)….???
kwakuwa mzazi/jamii huongea juu ya matokeo ya kusoma “soma uje upate maisha mazuri”..nakushau kueleza the beauty(uzuri ama utamu) wa mchakato wenyewe wa kusoma,
walimu hufundisha bila ku inspire,bila kutongoza hisia za wanafunzi, awe anauwaza mchakato wa kujifunza kila anapo lala, au kutembea na kutamani kuufanya kila siku.
NGOJA nieleze kidogo kwa mifano the baeuty(uzuri au sexiness) ya mchakato wa kusoma ili nieleweke nasema nini..(na maanisha mchakato the process sio masomo yenyewe)….(ni mawazo yangu lakini sio lazima niwe sahihi)
Nianze na “Kukariri” kama sehemu kubwa ya mchakato wa kusoma Tanzania.
..mwanafunzi Anapokuwa ana kariri masomo yake…pia kuna uwezo anaujenga ndani yake(kuna utamu wake)….mfano mimi kukariri kunaniwezesha leo nakariri nyimbo zaidi ya ishirini kichwani, naweza kuandika wimbo kichwani bila peni wala daftari, kukariri kutakusaidia kuja kuwa bingwa wa kutowa hotuba (speech) bila kusoma, kutakuwezesha kufanya presentation nakadhalika….mwanafunzi anapo kariri atambue pia anajijenga akitambua hivyo hata chukia hilo zoezi,
“KUANDIKA NOTES”
Unapoandika notes wakati mwalimu anafundisha…ndio kujifunza kuja kuwa mwandishi wa habari, msaidizi wa raisi ama waziri, ama msaidizi wa boss, ama kuwa mtafiti….mwanafunzi akijuwa hili atapenda zaidi na zaidi kuwa anaandika notes,
“KUSOMA KITABU”
Unaposoma kitabu….haijalishi unasoma nini…unajenga uwezo wa ku focus na kuko concentrate …hii ni skills muhimu sana maishani, inahitajika kwenye biashara, jeshini, michezoni, sanaa,dini, kwenye mahusiano nakadhalika
“KUFANYA assignment”
Mfano Unapo solve hisabati, fizikia, bookkeeping….una jenga uwezo wa kutatuwa matatizo….na kulingana na world economic forum hii ndio skills namba moja inayohitajika duniani….mwanafunzi asijione tu kuwa ana fanya hesabu ,bali anajijengea uwezo wa kutatuwa matatizo mbali mbali ambao sasa nchi,makampuni,mapenzi,jamii, familia zina uhitaji mkubwa sana wa watatuzi wa matatizo
“Kusikiliza mwalimu” anapofundisha….kuwa na uwezo wa kuskiliza (active listening…hii pia kulingana na world economic forum ni skills namba 9 katika skills zinazohitajika duniani….ukiweza kuskiliza kwa makini unaweza kuwa mbunifu wa masoko, mboresha huduma, mtunzi mzuri, mshauri au kiongozi…..so mwanafunzi atambue anapo mskiliza mwalimu yeye pia ana jijenga kiuwezo.
LAKINI pia kama alivyo wahi kusema Obama, mchakato wa kusoma humwezesha binadamu kuweza kutambua vipawa vyake….hutoweza kujijuwa wewe ni mwandishi mzuri kama huta andika pepa ya histori, au ushairi, hutajijuwa wewe ni mbunifu kama huja fanya project za shule, huja chora ramani, utaweza kujuwa wewe ni mwana harakati kwa ku fall in love na hadithi za kina mkwawa nakadhalika
Wanafunzi ni lazima wafundishwe na kuoneshwa namna mchakato wa kusoma ulivyo mtamu, ulivyo sexy, na unavyoweza kuwasaidia kujibu maswali yao ya msingi ya maisha yao kila siku, itakavyo wawezesha kutambuwa vipawa vyao na kuvikuza, ..Hapa msukumo wa kusoma utakuwa mkubwa na ufaulu nao utaongezeaka
Karibu ujiunge na familia yetu kama unaamini katika haya….MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES. 0715 200 900
Twitter: @chokadj @djchokatv
Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic
Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic
Download DJChokaMusic Android Application Click HERE
Comments
0 comments
Tags
DjChokaMusicNikki Wa Pili
InShare
Mkasi | S15E07 with Flaviana Matata Extended Version
ABOUT DJCHOKA
Related posts
Comments Off on Mkasi | S15E07 with Flaviana Matata Extended Version
Mkasi | S15E07 with Flaviana Matata Extended Version
Mkasi | S15E07 with Flaviana Matata Extended ...
23/02/2016 Comments Off on Listen/Download | NEW AUDIO: Snura – CHURA
Listen/Download | NEW AUDIO: Snura – CHURA
Listen/Download | NEW AUDIO: Snura – CHURA
23/02/2016 Comments Off on Listen/Download | NEW AUDIO: Pink ft Mr Blue – MUSIC (Prod Mbezi)
Listen/Download | NEW AUDIO: Pink ft Mr Blue – MUSIC (Prod Mbezi)
Listen/Download | NEW AUDIO: Pink ft Mr ...
23/02/2016 Comments Off on Listen/Download | NEW AUDIO: Roma (@Roma_Mkatoliki) ft. Walter Chilambo – MTOTO WA KIGOGO
Listen/Download | NEW AUDIO: Roma (@Roma_Mkatoliki) ft. Walter Chilambo – MTOTO WA KIGOGO
Listen/Download | NEW AUDIO: Roma (@Roma_Mkatoliki) ft. ...
23/02/2016
Yatosha
rss
Website Design & Hosting by Yatosha Web Services - + 255 783 36 16 80
Yatosha Web Servicesfree vector
0 MAONI YAKO:
Post a Comment