February 25, 2016

                          
Msanii mkongwe Mr Nice amesema ameshindwa kuitoa video yake ya wimbo Kioo kutokana na kuwa chini ya kiwango hali ambayo amedai ingemshushia heshima yake.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema tayari ameshashoot kazi mpya ambayo itatoka ikikamilika.
“Video ya Kioo ilikuwa tayari sema tumeshindwa kuitoa mimi na management yangu kutokana na kuwa chini ya kiwango. Kwa hiyo tukashauriana na watu wangu wa karibu tukaona hii sio kazi ya kwenda kwa jamii. Hivi sasa tayari tumeshoot nyingine kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Mr Nice. Pia Mr Nice alisema hayupo kwa ajili ya kushinda na wasanii wengine kwani yeye tayari alishafanya vitu vikubwa kwa wakati wake.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE