February 20, 2016

                      
Museveni ameongoza Uganda kwa miaka 30

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.Rais Museveni alipata kura5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.

Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.

Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE