Msanii maarufu kutoka nchini Jamaica Alaine yupo barani Afrika tangu wiki iliyopita. Kati ya mambo atakayoyafanya akiwa Afrika ni pamoja na kuzindua album yake mpya nchini Kenya,kwa sasa msanii huyo yupo Bongo
Nay wa Mitego ameshare picha hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa Studio ya WCB na Diamond, Alaine, Tudy Thomas na meneja wa Diamond, Sallam.
‘’Tuko kwenye mipango ila naomba hiyo ishu uiache kwa sasa kuna vitu tunaweka sawa tutalizungumzia wakati ukifika’’Nay
Hii ni mara ya pili Alaine kuja Bongo, mara ya kwanza ilikua ni 2013 kwenye Fiesta ya Dar es Salaam
Source: cloudsfm.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment