Baada ya Nay Wa Mitego kuimba kwenye ngoma yake mpya Shika Adabu Yako kuwa Ray anajichubua na anaishi nyumbani kwa wazazi wake,Ray amefunguka zaidi kupitia Leo Tena.
‘’Mimi sijichubui nakunywa sana maji na kufanya mazoezi namshangaa sana Nay kuniambia natumia pesa zangu za mauzo ya filamu kununua mkorogo sio kweli ni maisha tu ndio yamenibadilisha namshukuru Mungu sipingwi na jua ndani ya gari kuna AC,nyumbani AC na ofisini AC lazima uwe mweupe,’’Ray.
‘’Maisha ya zamani ya wasanii ni tofauti na sasa zamani msanii alikutembea juani kwa muda mrefu ndio maana tulikuwa tunaonekana weusi,Halafu sisi kwetu hatuna asili ya weusi ni maji ya kunde ,’Ray.
‘’Ni kweli naishi nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina nyumba na kuishi nyumbani sio dhambi ,kujitegemea ni maamuzi yako binafsi,mimi naishi nyumbani na mama yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi kujionyesha nina utajiri gani sipendi kupost mali zangu,sijui nina nyumba ,magari ni ishu zangu binafsi,kila msanii ana stlye yake ya maisha mwingine anapenda kujionyesha kwenye mitandao na mali gani,’’Ray.
KUHUSU CHUCHU HANS.
‘’Mpenzi wangu anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwetu,mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na mimi nyumbani kwangu,Chuchu Hans anajua kuhusu hili hata nyumba anaishi nimempangia mimi,uwezo wa kupanga ninao lakini mama yangu hapeni nihame nyumbani kwetu,Nampenda Chuchu kwa kuwani mpambanaji,’’Ray.
Source: cloudsfm
0 MAONI YAKO:
Post a Comment