February 04, 2016

                   
   Familia ya Abdul Bajandar ilishindwa kugharimia matibabu yake

Serikali ya Bangladesh imesema itagharimia upasuaji wa kumtibu mwanamume ambaye anaugua ugonjwa unaofanya mtu kupata dutu zinazofanana na mizizi ya mti mwilini.

Waziri wa afya wa Bangladesh Mohammad Nasim alitangaza hilo baada ya kumtembelea Abul Bajandar, hospitalini Alhamisi.

Bw Bajandar anaugua ugonjwa ambao kisayansi unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi.

Ni ugonjwa wa kinasaba ambao humfanya mtu kuota vidutu kwenye ngozi. Hujulikana sana kama “ugonjwa wa binadamu mti”.

Alianza kuota vidutu miaka 10 iliyopita.

“Awali, nilidhani hazina madhara,” Bw Bajandar ameambia AFP.


AFP

"Sasa zimeongezeka na nyingine zina urefu wa inchi mbili hadi tatu katika mikono yangu miwili. Kuna nyingine miguuni,” amesema.

Bw Bajandar alisafiri India kutafuta matibabu lakini familia yake haingemudu gharama.

Sampuli za damu yake na ngozi zitapelekwa kwenye maabara moja Marekani kuchunguzwa zaidi, profesa Abdul Kalam, ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa ngozi ameambia BBC.

Atatibiwa nchini Bangladesh baada ya matokeo ya uchunguzi kutolewa.

Bw Bajandar ni mmoja wa watu watatu wanaougua “ugonjwa wa binadamu mti” duniani, mkurugenzi wa hospitali ya chuo cha Dhaka, Samanta Lal Sen ameambia AFP.

Ni mara ya kwanza kwetu kupata kisa kama hicho hapa Bangladesh.


Source:BBC

Related Posts:

  • NEW AUDIO/ BIO ft MR BLUE - NISEME  Kama unaikumbuka analamika, Bibi, kaniulizia na baadhi ngoma toka kwakE. Anaitwa BIO hapa kamshirikisha MR:BLUE mzigo unaitwa Niseme. SKILIZA KISHA WAWEZA KU SHARE … Read More
  • YALIYOJILI DIVA SELFIE INSTAGRAM PARTY JANA     Ni usiku wa kuamkia leo ambao ulikua ukihusisha wanafamilia wote wa instagram walikutana ndani ya Club Bilicanas kwa ajili ya kupiga picha pamoja zile ishu za selfie ndiyo zilikua zikihusika sana. Kulikua… Read More
  • NANDO: NIPO TAYARI KUMUOA LULU Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa (the chase) 2013, Amir Nando ameweka wazi kuwa hajawai kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanadada wa filamu, Elizabeth Micheal aka Lulu, lakini anakubali sana. Akiz… Read More
  • MAAJABU YA NAY WA MITEGO, AJIPA ZAWADI YA GARI Jana ilikuwa ni Siku ya Kuzaliwa kwa Mwanamuziki Ney wa Mitego na aliamua kufanya sherehe kwa mara ya kwanza kusherehekea siku hiyo kwa vile huu ndio mwaka wake wa kwanza kuwa na mafanikio katika muziki , Ney alian… Read More
  • MUME WA FLORA MBASHA ALIA NA MCHUNGAJI GWAJIMA Na Makongoro Going’ MUME wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa miaka 17 (jina lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE