February 29, 2016



KAMATI ya Utendaji ya Klabu ya Simba imemsimamisha nahodha wake msaidizi Hassan Isihaka kuichezea klabu ya Simba kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya beki  huyo kumtolea maneno yasiyo na staha kocha wa Simba Jackson Mayanja kabla ya mechi ya jana Jumapili ya kombe la FA dhidi ya Singida United ambapo Simba ilishinda bao 5-1, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kutokana na kitendo hicho kisicho cha kiungwana kilichofanywa mbele ya wachezaji wenzake na kinachokiuka waraka wa maadili (code of conduct), Kamati ya utendaji licha ya kumsimamisha mchezaji huyo pia imeagiza alipwe nusu mshahara katika kipindi chote cha adhabu yake.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Simba, Haji Manara, imewataka wachezaji wote kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote wanapoitumikia klabu ya Simba.

Related Posts:

  • Wanawake wakatazwa kushabikia mechi   Wanaharakati nchini Iran wamekasirishwa na hatua ya kuwazuia wanawake nchini humo kushabikia mechi ya mpira wa wavu ya wanawake dhidi ya Marekani licha ya hakikisho kuwa wangeruhusiwa. Kumekuwa na ripoti kwamba … Read More
  • Mainda aanika kinachoua sanaa   BILA kuwataja kwa majina, msanii wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kitendo cha baadhi ya wasanii wanaojiona wamefikia vilele vyote vya mafanikio na kuwafanyia roho mbaya wenzao, ndiyo moja kati ya sabab… Read More
  • Yanga : "Kaseja Huru"   Ungozi wa klabu ya Yanga umesema hauna tatizo na golikipa Juma Kaseja endapo atataka kujiunga na timu nyingine yoyote ambayo ipo tayari kumsajili kwa ajili ya kuitumikia kwasababu kwa sasa mchezaji huyo hayupo k… Read More
  • Neymar kuikosa Copa America, afungiwa mechi nne na faini   Nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne kutokana na kitendo chake… Read More
  • CHADEMA Kilosa yapinga wananchi kuchangishwa pesa   Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kimesema hakuna sababu wananchi kubebeshwa mizigo ya michango isiyoisha wakati wanakabiliwa na changamoto za kukosa huduma za afya na ma… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE