February 17, 2016

                      
Beyonce na wacheza densi wake waliovalia kama wanachama wa Black Panther

Waandamanaji watatu walijitokeza katika mkutano wa kumpinga nyota wa muziki Beyonce nje ya uwanja wa soka ya Marekani mjini New York.

Maandamano hayo yaliitishwa baada ya onyesho la msanii huyo wakati wa mapumziko ya mechi katika uwanja huo ambapo yeye na wacheza densi wake walivalia kama wanachama wa kundi la itikadi kali la Black Panthers.

Watu wengi nchini Marekani walisema kuwa onyesho hilo lilikuwa pigo kwa maafisa wa polisi pamoja na wale wanaoshinikiza sheria kufuatwa.

Lakini kulikuwa na waandamanaji wengi wa kumuunga mkono Beyonce katika maandamano hayo.

                       
Wacheza densi wa Beyonce

Onyesho hilo la Beyonce mapema mwezi huu lilishirikishi wacheza densi waliovalia kama wanachama wa kundi la Black Panther.

Kundi hilo lilikuwa la wapiganaji wa haki za weusi nchini Marekani kati ya mwaka 1960 na 1980.

Wakati mmoja kundi hilo la Beyonce lilitengeza umbo la X,ambalo wengi wanafikiri lilikuwa la kumuenzi mwanaharakati wa haki za kijamii nchini Marekani Malcom X ambaye alipigwa risasi mwaka 1965.

Related Posts:

  • Aliyebaka mtawa akamatwa   Polisi nchini India wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kuhusiana na ubakaji wa mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki katika makaazi ya watawa Magharibi mwa Bengal. Viongozi wa Kikristo nchini India wamekosoa Serikali kwa k… Read More
  • CCM wamuonya Nape kauli zake kwa Lowassa   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki, amemtaka K… Read More
  • Maharamia waziteka meli mbili za Iran    Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mihadarati na Uhalifu kimesema kuwa maharamia wameteka meli mbili za Iran za kuvua samaki katika ufuo wa Somalia. Utakeji huo ni wa kwanza kufaulu tangu mwaka … Read More
  • CUF waitaka tume ya Taifa kukili kushindikana kwa kura ya maoni Naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kuhusu mchakato mzima wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa kielecron… Read More
  • Msilipize kisasa: Malim Seif Katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif amewaasa wanachama wa cuf jimbo la Dimani kutolipiza kisasi kwa kitendo cha kuchomewa moto ofisi yao usiku wa kuamkia juzi. Maalim Seif ambaye ni makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE