March 03, 2016

Krasnov 


Mwanamume aliyeandika kwamba hakuna Mungu katika majibizano mtandaoni ameshtakiwa kusini mwa Urusi.
Viktor Krasnov aliripotiwa kwa polisi na wanaume wawili waliokasirishwa na lugha aliyoitumia wakati wa majibizano katika mtandao wa kijamii wa Kirusi wa VKontakte mwaka 2014.
Mtandao huyo hufanana sana na Facebook na ni maarufu sana.
Ameshtakiwa Stavropol kwa kosa la "kutusi hisia za waumini”.
"Matusi” kama hayo yaliharamishwa kisheria mwaka 2013 baada ya kesi ya Pussy Riot.
Wakati wa majibizano hayo, Bw Krasnov anadaiwa pia kupuuzilia mbali Biblia na kusema ni “mkusanyiko wa hadithi za kubuni za Wayahudi”.
Wataalamu wa lugha waliunga mkono msimamo wa Bw Krasnov kwamba maandishi yake yalikuwa “matusi kwa waumini” hao.
Kwa mujibu wa sheria ya Urusi, akipatikana na hatia, anaweza kufungwa jela mwaka mmoja na kutozwa faini ya hadi $4,083) au kufanyishwa kazi ngumu saa 240

Related Posts:

  • FIESTA2017 yazinduliwa rasmi   Kile kitendawili kilichokuwa kikiumiza vichwa vya wengi vya uwepo wa tamasha la Fiesta 2017, sasa kimeteguliwa rasmi . Tamasha la Fiesta ambalo huvutia umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali nchini, limezind… Read More
  • Brand New Vide: Chovya - Dayna Nyange   Baada ya kukaa kimya kwa takliban mwaka mmoja bila kuachia wimbo, mwanamuziki Dayna Nyange ametuletea video ya wimbo wake mpya kabisa unaitwa Chovya. Katika Video hiyo Dayna Nyange pia ameonekana mdogo wa mwanamu… Read More
  • Rais Buhari arejea nyumbani   Abuja, Nigeria Baada ya kukaa takribani miezi mitatu akipatiwa matibabu nchini Uingereza hatimaye Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewasili katika mji mkuu wa Abuja na kupokelewa na viongozi wa ngazi za juu wa … Read More
  • Brand New Video: Sal Houdini ft Rihanna- I Just   Mambo vp mpenzi wa ubalozini.blogspot. Tunakuletea wimbo mpya kabisa uliowakutanisha wanamuziki Rihanna na Sal Houdini wakikwambia I just. Video ya wimbo huo tumekuwekea hapa chini, fanya ku bofya play kwa ajili … Read More
  • Mfahamu muimbaji na mtunzi wa kwanza wa wimbo maarufu wa Malaika   Tunamini kabisa unaufahamu wimbo maarufu wa afrika wa Malaika. Wimbo wa Malaika umeimbwa na wasanii wengi sana wakubwa kwa wadogo, Mailaka uliimbwa na Boney M, Miriam Makeba, King Crazy GK na mwanamuziki Ainea pi… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE