Serikali
imewasimamisha kazi Maafisa 3 wa Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa
tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya Ndege na mmoja kati yao kuiba
mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kampuni ya
Swissport.
Akizungumza
katika Ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika Viwanja vya Ndege vya
Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa mambo ya ndani
Mh.Mhandisi Hamad Masauni amewataja walio simamishwa kazi ni Khalfani
Kisana na Mussa Mandauli ambao walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya
Ndege wakiwa na gari la Serikali lenye usajiri STJ 2948 huku askari
mwingine aliyejulikana kwa jina la Abas Mwanza akishutumiwa kwa kosa la
kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport |Lucas Maganda kwa kosa la kuiba
mzigo wa abiria.
Akiwa
katika kiwanja hicho Mh.Masauni amekagua utendaji kazi katika idara ya
Uhamiaji,Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza viongozi wa idara hizo
zilizopo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote
atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment