RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kewe Mama Janeth Magufuli leo asubuhi wameiingiza Clouds TV katika historia pekee ya kuwa ndiyo kituo cha kwanza cha habari kupigiwa simu live na Rais wa nchi na kuwapongeza kwa kile wanachokifanya.

Rais Magufuli na mkewe mama Janeth wamepiga simu moja kwa moja katika kipindi cha Clouds 360 na kuwapongeza watangazaji wa kipindi hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Rais Magufuli alisema kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kituo hicho na anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Clouds Media Group kama zoezi zima la ‘Malkia Wa Nguvu’ na mengine mengi. Wakiongea na watangazaji wa Clouds 360, waliwataka nao wakati mwingine waje na wenzi wao katika kipindi na si kila mara waje wenyewe .
Wafanyakazi wa kituo hicho walimshukuru rais kwa kitendo chake hicho chenye kuonyesha kuwa wanaifanya kazi yao vizuri lakini pia wanasema ilikuwa faraja kwao kwani wanaamini kituo hicho kimekuwa cha kwanza kwa rais kufanya kitendo hicho.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment