Ahadi ni deni. Ndugu mdau , tulikuahidi kukuletea historia ya filamu ya maisha ya Yesu na kukujuza juu ya yule bwana aliyeigiza ndiyo yesu. Kesho ni siku kuu ya Pasaka. Wakristu ilimwenguni wanasherehekea ufufko wa bwana wao yesu kristu.Ni jambo la kawaida kukuta nyumba za waumini wa dini ya Kikristo zikiwa zimepambwa na picha mbalimbali za Yesu, lakini pia kama wewe ni muumini wa dini hiyo, unapotajiwa au kulisikia jina la Yesu, kuna picha fulani inakujia mawazoni, kuna sura fulani inakujia mawazoni, si picha au sura nyingine, bali ni sura ya Yesu.
Wapo wanaodhani kuwa picha hiyo au sura hiyo ndiyo Yesu mwenyewe aliyezaliwa yapata miaka 2016 iliyopita, hapana, hakuna anayejua sura ya Yesu ikoje, anaonekana vipi, bali mtu huyo ambaye ulimwengu umezoea kumwona kama ndiyo Yesu wa Nazareti, huyu ni jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Brian Deacon, huyu ndiyo jamaa aliyeigiza ile filamu maarufu ya Yesu, inayojulikana kwa jina la ‘Jesus Film’ mwaka 1979. filamu hiyo iliigizwa na watu mbalimbali ambao wengine wapo hai mpaka leo, picha za filamu hiyo zilipigwa nchini Israeli.
Je Brian Deacon ni nani?
Brian Deacon ndio jina halisi la mwigizaji huyo ambaye ni raia wa Uingereza alizaliwa tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza ni mtoto wa pili katika familia yao, baba yake alikuwa ni fundi makenika huku mama yake akiwa akiwa ni Muuguzi.
Brian Deacon aliyegiza kama yesu katika filamu ya Yesu
Maisha yake ya Ndoa
Brian alifunga ndoa yake ya kwanza na binti
aliyejulikana kwa jina la Rula Lenska mwaka 1977 na kufikia mwaa 1987
ndoa hiyo ilivunjika, huku wakiwa wamefanikiwa kupata mtoto wa kike
ajulikanaye kwa jina la Lara Deacon,
Mwaka 1998 alifunga ndoa nyingine baada ya kuachana na Rula, alimuoa Natalie Bloch ambaye yupo naye mpaka sasa.
Alipata nafasi ya kuigiza filamu ya Yesu baada ya kupita mchujo, katika mchujo huo walijitokeza waigizaji zaidi ya 1000. Brian Deacon aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, filamu hiyo ya Yesu ilimfanya yeye kuokoka baada ya kuitamaza kwani kabla ya kuigiza filamu hiyo hakuwa ameokoka. ilichukua miezi saba Mpaka filamu hiyo inakamilika
Filamu nyingine alizowai kucheza ni kama A Zed & Two ( 1985), Vampyres ( 1974 ), The Triple Echo ( 1972) , Lillie (1978) SOURCE : venancefuraha.blogspot
kiwa
leo ni Ijumaa kuu,siku ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka mateso
ya mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka
2000 iliyopita.Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu
ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS''
ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya
hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa
maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu
aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye
amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa
yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye
si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU. - See more at:
http://www.gospelkitaa.co.tz/2012/04/mjue-mwigizaji-wa-filamu-ya-yesu-ambaye.html#sthash.aqhMkLAC.dpuf
Ikiwa

0 MAONI YAKO:
Post a Comment