Leicester wameshangaza wengi msimu kwa kukwamilia kileleni
Klabu ya Leicester City ya Uingereza itacheza dhidi ya miamba wa Ulaya, klabu ya Barcelona kutoka Uhispania, Agosti mwaka huu.
Klabu hiyo zitakutana katika dimba la Kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambalo huchezwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Viongozi hao wa Ligi ya Uingereza pia watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.
Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL
Leicester watakutana na Celtic mjini Glasgow tarehe 23 Julai, PSG mjini Los Angeles tarehe 30 Julai na Barcelona mjini Stockholm tarehe 3 Agosti.
Barcelona ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya
Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu tano za Ligi ya Uingereza zitakazoshiriki michuano hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa huchezewa Marekani.
Klabu nyingine kutoka Uingereza ni Manchester United, Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspur.
Msimu mpya wa Ligi ya Premia utaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti.
Ratiba ya Mechi za Klabu Bingwa Kimataifa
23 Julai - Celtic v Leicester, Glasgow24 Julai - Inter v PSG, Eugene27 Julai - Real Madrid v PSG, Columbus27 Julai - Bayern Munich v AC Milan, Chicago27 Julai - Chelsea v Liverpool, Pasadena30 Julai - Celtic v Barcelona, Dublin30 Julai - Inter v Bayern Munich, Charlotte30 Julai - AC Milan v Liverpool, Santa Clara30 Julai - PSG v Leicester, LA3 Agosti - Barcelona v Leicester, Stockholm3 Agosti - Bayern Munich v Real Madrid, East Rutherford3 Agosti - AC Milan v Chelsea, Minnapolis(Kuthibitishwa baadaye) - Liverpool v Barcelona(Kuthibitishwa baadaye) - Inter v Celtic(Kuthibitishwa baadaye) - Real Madrid v Chelsea
0 MAONI YAKO:
Post a Comment