Staa wa muziki kutoka nchini Marekani, Mariah Carey ambaye kwa sasa anafanya ziara katika bara la Ulaya, Sweet Sweet Fantasy European Tour ameghairi kufanya shoo leo Jumapili, shoo ambayo ilikuwa inatarajiwa kufanyika Brussels, Ubelgiji.
Mariah Carey ametoa taarifa ya kughairi kufanya shoo hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter ambapo aliandika kuwa kwa usalama wa watu ambao anafanya nao kazi ameamua kughairi kufanya shoo hiyo na badala yake itapangwa siku nyingine,
“Ninawapenda mashabiki wangu wa Brussels na kwa muda huu nimeghairi shoo yangu kwa ajili ya usalama wa mashabiki wangu, bendi yangu, timu nyangu nzima na kila mtu ambaye alikuwa katika ziara yangu” aliandika na kuongeza “Ninamatumaini kuja hivi karibuni na ninawaombea kwa upendo, kicheko na mwangaza kwa watu wa aina zote”
Aidha taarifa hiyo hakikuelezea ni jinsi gani mashabiki waliokuwa tayari wamenunua tiketi kwa ajili ya shoo hiyo ambayo pia Mariay Carey anasherekea siku ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 46 watafidiwa vipi pesa zao.