Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyemaliza muda wake , Dk Rajab Rutengwe amemuomba msamaha Rais Dr Magufuli na kumuomba msaada amfikirie upya kutokana na kutokujua ashike wapi tangu alipomuachisha kazi hiyo .
Dk Rutengwe amesema tangu aachishwe kazi amepoteza mwelekeo huku akiwa ni tegemezi katika familia masikini.
Aliongea hayo alipokuwa anakabidhi ofisi kwa Mkuu mpya wa mkoa huo Dk Kebwe ambapo alitumia wasaa huo kuwaomba msamaha wana Morogoro , familia yake na watanzania kwa ujumla huku akisema hajui amekosea wapi .
Dk Rutengwe alizungumza hayo kwa huruma na hisia kali na kuwafanya baadhi ya viongozi na waandishi wa habari kutokwa machozi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment