March 12, 2016


Mlipuko nje ya Banki Kuu ya Nigeria  
 
Mlipuko umejiri nje ya jengo la Banki Kuu ya Nigeria katika mji wa Calabar kusini mwa nchi hiyo na kupelekea watu wasiopungua wawili kuuawa na wengine 18 kujeruhiwa Ijumaa.
Msemaji wa polisi katika jimbo la Cross River, John Elu amesema yamkini mlipuko huo umesababishwa na silinda ya gesi.
Nigeria iko katika hali ya tahadarhi kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Magaidi wa kundi hilo wamewaua watu karibu 20,000 tokea mwaka 2009 na kupelekea zaidi ya milioni mbili kukimbia makaazi yao katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Idadi ya waliopoteza maisha baada ya jengo lenye ghorofa 5 kuporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos imepindukia 30.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imesema kuwa, jengo hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa liliporomoka Jumanne iliyopita, kutokana na ukiukaji wa kanuni za ujenzi.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE