Mtoto
wa siku moja ameibwa katika mazingira ya kutatanisha katika Hospitali
ya Rufaa ya Bugando, akiwa pembeni mwa mama yake aliyekuwa amelala,
mwenye umri wa miaka 16.
Akizungumzia
uporaji huo jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Justus
Kamugisha, amesema aliyepora mtoto huyo aliingia ndani ya wodi ya wazazi
ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando, akiwa amejifunga ushungi.
“Alipoingia
wodini alikuta mama wa mtoto amesinzia akiwa peke yake wodini, ndipo
akamuiba mtoto wake wa kike mwenye umri wa siku moja na kuondoka naye
kwenda kusikojulikana,” alisema.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kamugisha, Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa
tukio hilo kwa kuhoji wauguzi, walinzi na wazazi waliokuwa wamelazwa
wodini hapo.
Katika
hatua nyingine, Kamanda Kamugisha amesema Jeshi la Polisi mkoani humo,
litaanza kufanya uhakiki wa silaha kuanzia Aprili mosi hadi Juni 30
mwaka huu, katika ofisi za makamanda wa Polisi wa wilaya zote za Mkoa wa
Mwanza.
Amesema
uhakiki wa silaha ni wa kitaifa na utahusu wamiliki binafsi, kampuni
binafsi na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali
zinazomiliki silaha.
“Lengo
ni kupata kumbukumbu ya uhalali wa umiliki wa silaha. Watu wote
wanaomiliki silaha watii agizo hili bila kulazimishwa, ili tufanikishe
uhakiki kwa wakati na tuimarishe usalama katika mkoa wetu,” alisema.
Aliwataka
watu wanaomiliki silaha isivyo halali, kusalimisha silaha hizo wenyewe
kwenye ofisi za Serikali na kwa wakuu wa Polisi wa wilaya (OCD) kabla ya
muda wa uhakiki wa silaha kumalizika.
“Baada ya hapo tutafanya msako kabambe wa watu waliokaidi kuhakiki silaha zao,” alisema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment