March 18, 2016

                     
MKAZI wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda  kupatiwa matibabu kwa kaka yake.

Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.

Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.

Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).

Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.

Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.

Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.

Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.

Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.

Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.

“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama   alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,”alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.

Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.

Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia msiba huo, mume mkubwa alisema kuwa amepata pigo kubwa kwa sababu alikuwa anasaidiwa mno na marehemu Veronica kutokana na biashara zake za pombe za kienyeji ambazo zilisaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Veronica aliugua muda wa miezi miwili, nilikuwa namplekea Kituo cha Afya Urwila kupata matibabu, lakini Mungu kampenda zaidi,” alisema.

Related Posts:

  • Venus Williams apigwa chini katika tenisiKonta ameorodheshwa nambari 47 duniani Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi la Australian Open mjini Melbourne. Konta, 24, al… Read More
  • Criss wamarya amerudi na Madee wakikwambia Pepea Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya toka mkoani Morogoro Criss wamarya, baada ya kutamba na nyimbo zake za kilomita sita, sinyorita, tutoke na Cheusi mangala na hatimaye akakaa kimya kwa muda, amekuja tena na wimbo wak… Read More
  • Brand New Audio | Nipe Tamu - Every Day    Mwanamuziki chipukizi kabisa kutoka mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina la Every Day, amekuletea bonge ya wimbo wake unaoitwa Nipe Tamu. Wimbo umefanywa na Producer Sniper katika studio za Tushi Recordz za… Read More
  • New Video | Nalia - H- Kubwa    H-Kubwa anakukaribisha katika video yake mpya inayotwa Nalia. Hapa amemshirikisha mwana dada  Elumai             … Read More
  • Ashtakiwa kwa kusambaza picha whatsapp         Miili ya kwanza ya wanajeshi waliouawa Somalia iliwasili Nairobi Jumatatu Mwanamume mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kusambaza picha alizodai ni za wanajeshi wa Kenya waliouawa … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE