March 19, 2016

Wanaharakati wa haki za binaadamu na jumuiya za waandishi wa habari nchini Tanzania hivi leo zimetoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa mwandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi Communications na mwakilishi wa Deutsche Welle visiwani Zanzibar, Salma Said, ambaye ametoweka tangu jana katika mazingira ya kutatanisha. Kwa upande wake, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini humo, UTPC, umesema unapingana na kitendo hicho ambacho umesema kinarejesha nyuma jitihada za waandishi kufanya kazi zao. Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan, ameiambia DW kwa njia ya simu kwamba kukamatwa kwa Salma katika mazingira yasiyoeleweka ni hatari kwa uhuru wa habari. "Huku ni kumtisha ili asifanye kazi yake ya uandishi kwa haki na uadilifu na haikubaliki. Serikali inaonekana kutumia nguvu sana dhidi ya waandishi kama yeye na hivyo si sawa. Tutasimama pamoja naye na tunataka aachiliwe mara moja," amesema Abubakar Karsan. Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wa Facebook hivi leo, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binaadamu nchini humo, THRD, umesema unalaani vikali kutekwa kwa mwandishi huyo wa kike na kuvitolea wito vyombo vya usalama "kutoa ushirikiano katika kipindi hiki" na pia kuwataka waandishi wa habari "kuungana ili kushinikiza" apatikane haraka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE