Waziri wa Nishati wa Kenya, Cherles Keter, na ujumbe wake amezuiwa kuingia katika bandari ya Tanga.
Kutokana
na hatua hiyo, serikali mkoani Tanga imetoa ufafanuzi kuhusu kuzuiwa
kwa waziri huyo na ujumbe wake wa watu 13 kuwa kulitokana na kutokuwa na
taarifa za ujio wao.
Keter
na maofisa wake wandamizi wakiwamo makatibu wakuu, walijipenyeza wakati
wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.
Ujumbe
wa waziri huyo aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya
nchi hiyo, Joseph Njoroge na mwenzake wa masuiala ya petroli, Andrew
Kamau.
Vigogo
hao, waliokuwa wameongozana na maofisa mbalimbali akiwamo Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Usafirishaji wa Mafuta kutoka Lamu- Sudan
Kusini- Ethiopia (Lappset), Sylvester Kasuku, walizuiwa kwenye Uwanja wa
Ndege wa Tanga, baada ya kuwasili.
Muloni
na ujumbe wake, alitokea Kenya baada ya kukagua Bandari za Lamu na
Mombasa na aliingia nchini kukagua Bandari ya Tanga, ikiwa hatua ya
mchakato wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Ziwa Albert,
Uganda hadi Bahari ya Hindi.
Akizungumza
hatua hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga,
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa, Martin Shigella, alisema ujumbe wa Keter
ulizuiwa kutokana na kutokuwa na taarifa nao na kwamba walikuwa katika
viwanja vya ndege kwa ajili ya kungoja ugeni wa Waziri Muloni tu.
Shigella
alisema kuwa walishangazwa kuona ujumbe huo wa Kenya umekuja kufuatana
na waziri huyo bila kuwapo kwa taarifa yeyote ya awali ya ujio wao.
Keter
na maofisa wake waliwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga sambamba na
ujumbe wa Waziri wa Uganda, ambao wote kwa pamoja waliwasili kwa
helikopta nne, zilizotua kwa pamoja uwanjani hapo.
Baada
ya kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na baada ya Waziri
Muloni kumaliza ukaguzi wa Bandari ya Tanga na maeneo ambayo yametengwa
kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, iwapo mradi huo utaridhiwa
kutekelezwa na serikali ya Uganda, ujumbe huo uliruhusiwa kuondoka.
Hata
hivyo, serikali ya Uganda ilieleza kuridhika kwake baada ya kuona hali
halisi ya mazingira ya Bandari ya Tanga ikiwa hatua mojawapo ya mchakato
wa awali wa ukaguzi kabla ya kupitishwa makubaliano ya ujenzi wa mradi
huo.
Kutokana
na hatua hiyo, serikali hiyo inatarajia kutuma timu ya watalaamu kutoka
Uganda ili kufanya ukaguzi wa kina kwenye Bandari ya Tanga, kubaini
uwapo wa vigezo vinavyotakiwa katika utekelezaji wa mradi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment