March 18, 2016


Raia milioni sita US wanakunywa maji yasiyo salama

Wamarekani milioni sita wanatumia maji ya kunywa yasiyo salama majumbani mwao na mashuleni ambayo yamechanganyika na madini ya risasi.
Ripoti iliyochapishwa na toleo la jana la gazeti la USA Today inaonyesha kuwa kulingana na kibali na agizo lililotolewa na serikali kuu ya Marekani Wamarekani wapatao milioni sita wanatumia maji ya kunywa yenye kiwango cha juu cha mchanganyiko wa madini ya risasi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo unaonyesha kuwa mifumo elfu mbili ya usambazaji maji nchini humo ina kiwango cha juu cha madini ya risasi zaidi ya inavyokubalika.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo, hivi sasa kuna mamia ya vituo vya malezi ya watoto pamoja na shule zinazotumia maji yaliyochanganyika na kiwango cha juu cha risasi. Ripoti hiyo imeongeza kuwa watoto wadogo wanakabiliwa zaidi na athari zenye madhara ya risasi ambayo ni aina ya sumu, kulinganisha na watu wa marika mengine. Madini hayo yanaathiri mishipa ya fahamu na yanaweza kudumaza moja kwa moja uwezo wa kujifunza mtoto na kusababisha pia matatizo ya kitabia.
Ripoti ya gazeti la USA Today inaonyesha kuwa katika majimbo yote 50 ya Marekani, kiwango cha risasi ndani ya maji ya kunywa ni cha juu zaidi ya inavyokubalika.../

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE