March 18, 2016

 

Jioni ya leo katika ukurasa wa facebook wa shirika la Habari la Ujerumani DW, wali andika juu ya kukamatwa kwa mwandishi wake aliyepo Zaznibar. Taarifa zilisomeka hivi

"Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa mwakilishi wetu visiwani Zanzibar, Salma Said (pichani), amekamatwa na watu wasiofahamika kwa sababu ambazo bado DW haijazielewa. Tumezungumza naye akiwa sehemu anayosemekana kushikiliwa na sikiliza kwenye matangazo yetu ya jioni"

Taarifa za jioni hii ambazo DW wamepost katika ukurasa wa Facebook zinasema hivi
 
"Wakati huu tukifunga matangazo yetu ya moja kwa moja kutoka hapa Bonn leo tarehe 18 Machi 2016, bado hatujuwi mwandishi wetu wa Zanzibar alipo, licha ya kumpata kwa simu ambayo baadaye ilizimwa. Tunaungana na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha wasiwasi kuhusu hatima yake. Tunafanya kila lililo kwenye uwezo wetu na tutawafahamisheni punde tu tutakapopata taarifa zinazomuhusu"


Ubalozini.blogspot.com tunaungana na famili ya DW katika kipindi hiki kigumu

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE