March 09, 2016

Tani 15,000 za korosho za magendo zakamatwa Ivory Coast
Maafisa wa Ivory Coast wameripoti kuzuia tani 15,000 za korosho za magendo zilizokuwa zikipangwa kusafirishwa Ghana kinyume cha sheria.
Mnamo tarehe 4 mwezi Machi, maafisa wa Ivory Coast pia waliwahi kukamata tani 10,000 za korosho zilizokuwa zikisafirishwa maeneo ya Bondokou na Transua yaliyoko mpakani mwa Ghana.
Eneo la Bondokou nchini Ivory Coast linatambulika kwa uzalishaji wa korosho na pia huendeshwa biashara za magendo kati ya nchi hiyo na Ghana.
Kwa kipindi cha miaka minne ya mwisho, serikali ya Ivory Coast imekuwa ikipambana dhidi ya biashara haramu ya korosho ambapo ilionekana kukithiri mwaka 2012 na kufikia tani 100,000.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE