March 14, 2016

                          
Wakuzaji bangi wakutana Israeli

Wataalamu wanaohusika na matumizi ya bangi kama dawa wanakutana Israel kujadili uvumbuzi zaidi katika kilichokuwa sekta yenye thamani ya mabilioni ya dola duniani.

Hayo ndiyo maazimio ya Canna-Tech inayojumuisha wawekezaji, wakulima halali na watumizi wa bangi kama dawa.

Uwekezaji katika sekta hiyo umekuwa kwa kasi ya juu mno kufuatia uhalalishwa kwa bangi katika majimbo kadhaa nchini Marekani.

Nchini Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia utafiti na uwekezaji mkubwa.

Afisa mmoja anayesimamia utafiti huo Saul Kaye anasema

''Wagonjwa ni watu wanaopata matibabu ya maradhi ambayo yanapatikana baada ya kutumia kemikali yenye madhara kama vile ugonjwa wa Saratani.

                          
Nchini Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia utafiti na uwekezaji mkubwa.

Watu hao ni wale wanaougua ugonjwa wa kusahau, ugonjwa wa Crohn, na wale walio na msongo wa mawazo au mfadhaiko.

Bangi inaweza kusaidia matatizo kama hayo, na bado hatujajua manufaa mengine.

Utafiti unahitajika zaidi, jambo ambalo Israeli inaendelea kuchunguza hasa katika ngazi ya shirikisho

Kwa sasa, kuna utafiti zaidi ya 36 unaoendelea katika hospitali nchini Israeli. ''

Biashara hii ya bangi iliyoanzishwa kwa njia ya soko la magendo, na wafanyibiashara wa awali walitokea hapo.

Lakini kuna kampuni mahususi ya uundaji madawa, katika soko la hisa la Wall Street Marekani sasa yanaangazia biashara ya bangi, hapo ndipo tunaivalia njuga, na bila shaka tunaanza kubadili mtizamo kuhusiana na biashara ya bangi.'' alisema Kaye

Related Posts:

  • DIAMOND ULINZI MZITO UGANDA, AWEKEWA WAJEDA Mlinzi kutoka jeshi la Uganda Hawa askari tuliwaona wakati Diamond Platnumz amewasili Uganda na kupokelewa Airport kwa mbwembwe sana. Kumbe ulinzi wao uliendelea mpaka siku ya sho ambapo mmoja wao aliwekwa Nje y… Read More
  • TUONANE JANWARY SHOW KUFANYIKA MORO JUMAPILIKama upo Morogoro tukutane uwanja wa K/NDEGE shule ya Msingi  jumapili hii tutakuwa na @officiallinah @fidq @staminashorwebwenzi @Shilolekiuno @yamotoband @Nikiwapili  @Mwanafa na list nzima hiyo hapo. Utakosaje sas… Read More
  • VIDEO YA ALLY KIBA KUONESHWA KWENYE VITUO HIVI VIKBWA Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’imeanza kuonyeshwa ijumaa ya 19 Decemba 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Video imeta… Read More
  • TIBAIJUKU AGOMA KUJIUZURU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo Akiendelea kuzungumza na waandishi muda huu anasema watu wanaona kujiuzulu ni 'fashion' ila … Read More
  • HATIMAYE FLORA MBASHA ADAI TALAKA Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha. Flora amefungua kesi ya mad… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE