Waziri mkuu Kasim Majaliwa ametoa siku kumi kwa watumishi wote wa halimashauri ya wilaya ya Busega akiwemo mkurugenzi wa Halimashauri hiyo Hamisi Yuna wanaoishi wilayani Magu kuhakikisha wanahamia wilayani hapo ifikapo march kumi na tano mwezi huu.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo alipokuwa akiwahubia wananchi wa kijiji cha Lamadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Kisesa.
Katika hatua nyingine waziri mkuu amewaonya wazazi wote katika wilaya hiyo watakothubutu kuwaachisha masomo kwa lengo la kuwaozesha waache mara moja kwani atakayebainika katika uongozi huu wa awamu ya tano atakiona cha moto.
Awali mbunge wa viti maalumu mkoa wa Simiyu Ester Midimu amemuomba waziri mkuu kumukumbisha rais magufuri ahadi yake aliyotoa ya kila kata kupewa shilingi milion hamsini ili wananchi waweze kujinasua kwa kuanzisha miradi.
Source:itv.co.tz
0 MAONI YAKO:
Post a Comment