March 17, 2016

Nape Nnauye

 Kufuatia kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini  bila kufuata Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa Filamu hizo leo jijini Dar es Salaam.
Amewataka wauzaji hao kuwa na  mkataba pamoja  wamiiki wa kazi hizo iliwaweze kufanya biashara hiyo kwa uhalali kwakua Serikali itawasaidia kusimamia utekelezaji wa mikataba hiyo na kurahisisha utekelezaji wa sheria iliyopo.
“Lazima mfuate na kutekeleza Sheria iliyopo kwakua mimi nipo hapa kuisimamia na kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa”.Alisema Mhe.Waziri Nape.
PIX 2
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao kati ya Serikali na wauzaji wa Filamu za nje(Hawapo Pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw Tairo.
Aidha katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo ameongeza kuwa nilazima wauzaji wa filamu hizo kuhakikisha kuwa filamu wanazouza zimehakikiwa na bodi ya filamu pamoja na COSOTA ili kudhihirisha ubora wa kazi hizo na viwango vya hapa nchini.
“Ni lazima muhakikishe kazi mnazouza zimeruhusiwa na Bodi ya filamu pamoja na COSOTA  na zinafuata  madili ya hapa nchini’’.Aliongeza Bi. Joyce.
Ameongeza kuwa bodi ya Filamu pamoja na COSOTA  wapo tayari kuwasaidia kupata haki miliki ya filamu hizo wanazouza kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kuruhusu filamu gani inastahili kuuzwa na ipi haistahili kuwepo sokoni.
 Uuzaji wa filamu za nje hapa nchini umechangia kwa kiasi kikubwa filamu za hapa nchini kukosa soko hali inayochangia kudidimia kwa sanaa hiyo hapa nchini ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana.
Imeandaliwa na Shamimu Nyaki


Joseph Lyakurwa
Mwenyekiti wa  wauzaji wa filamu za nje Bw Joseph  Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye wakati wa kikao baina ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.


PIX 4
Baadhi ya wauzaji wa Filamu za nje  walioshiriki katika kikao kati yao na Serikali cha kubadilisha sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini kilichofanyika leo jijjini Dar es Salaam.(Picha na Shamimu Nyaki).

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE