WAJUMBE
wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar leo
wamefanya Uchaguzi wa kumpata mjumbe atakaye peperusha bendera ya CCM
katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Spika wa Baraza hilo, kwa kipindi
cha mwaka 2015 - 2020.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa
Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu, amesema uchaguzi huo
ulioendeshwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,
ulifanyika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, uliojumuisha wajumbe 72, alimtangaza Zubeir Ali Maulid kuwa mshindi baada ya kupata kura 55 na kuwashinda wapinzani wake wawili aliyemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho aliyepata kura 11 na Jaji Janeth Nora Sekihola aliyepata 4, na kura mbili (2) ziliharibika.
Jumla ya wanachama tisa (9) walijitokeza kuomba ridhaa ya CCM ili wagombee nafasi hiyo ya Spika .
Katika
kikao cha Kamati Maalum kilichofanyika Machi 24, mwaka huu, Ofisi Kuu
ya CCM Zanzibar, ilipitisha majina matatu ikiwa ni pamoja na Pandu
Ameir, Zubeir Ali Maulid na Janeth Nora Sekihola, ambapo uchaguzi wake
umefanyika leo.
Akitoa
neno la shukrani, Zubeir Ali Maulid, aliwashukuru wajumbe hao kwa imani
yao kwake na kuwataka wampe kila aina ya mashirikiano ili aweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Naye
aliyekuwa Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho, amekubali kushindwa
na kumuahidi kumpa msaada wowote atakaohitaji, iwapo atatakiwa kufanya
hivyo.
Uchaguzi huo wa Spika unatarajiwa kufanyika mara tu baada ya kuitishwa kwa Baraza jipya la Wawakilishi.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Sgd
…………….
(Waride B. Jabu),
Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
25/03/2016.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment