Utawala katika jimbo la Minnesotta
nchini Marekani umekuwa ukitoa taarifa kufuatia uchunguzi wake kuhusu
kifo cha mwanamuziki Prince.
Utawala huo unasema kuwa hakuna
dalili ya kuumia kwenye mwili wa Prince ambao ulipatikana nyumbani kwake
karibu na Minneapolis siku ya Alhamisi.Unasema kuwa hakuna haja wakati huu kusema kuwa Prince alikuwa amejiua.
Msemaji wa wachunguzi (Martha Weaver) alisema kuwa uchunguzi kwenye maiti ya mwanamuziki huyo umekamilika na kwamba wameisalimisha maiti hiyo kwa familia yake.
Matokeo ya uchunguzi huo hayatarajiwi hivi karibuni.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment