April 09, 2016



Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad leo jumap[ili ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (leo) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Related Posts:

  • JOBFIRE A.K.A (SAUTI ZA MATUKIO) ASAKA MDHAMINIPICHANI NI MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA ANAYEJULIKANA KWA JINA LA JOBFIRE A.K.A SAUTI ZA MATUKIO,, NI MZALIWA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO ILA KAZI ZAKE KIMUZIKI ANAFANYIA KISIWANI ZANZIBAR, CHIMBUKO LAKE NI MKOA WA TANGA,… Read More
  • SELE CHID BEENZ BIFU ZITO    Msanii Afande Sele aligeuka mbogo baada kumjibu msanii mwenzake Chid beenz kuwa hawezi kumteka na hana uwezo huo kwani Afande ameshakua mwanajeshi JWTZ na akaacha jeshi hivyo awezi kutishiwa amani n… Read More
  • Mr.Blue kuitwa baba Hivi karibuni Ni Baada ya zile story zilizovuma na hatimae Byser mwenyewe kukubali kua anategemea kupata mtoto na mpenzi wake wa zamani sanaaa ambae anajulikana kama Wahda Mohamed....Sasa Nyota njema imeshaanza kuonekana ambapo mw… Read More
  • KUNDI LA BLUE 3 KURUDI TENA UPYAA..!! Ex Blu3 star who is now rumoured to be back to the group after they reunited with Jackie and Lillian has shown the other side of her by coming to the rescue of a one year old who was burnt by her father after a simple… Read More
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - TAMASHA LA MICHEZO TAMASHA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA SERIKALI YA UINGEREZA NCHINI KUPITIA SHIRIKA LA ‘BRITISH COUNCIL’ TAREHE: 27, MACHI, 2012MUDA: 4 Asb- 7… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE