Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Mhe.
James Mbatia ametoa msaada kwa wananchi wa jimbo lake kufuatia kutokea
kwa mafuriko katika jimbo hilo na wananchi kupatwa na majanga mbalimbali
hivyo kuhitaji msaada.

Diwani
wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi wa
Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata
hiyo kutizama athari zilizotokana namafuriko

Baadhi
ya wakazi wa kata ya Kahe wakiwa katika kikao na ujumbe wa Mbunge wa
jimbo la Vunjo uliofika katika kata hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa
chakula.

Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Michael Kilawila akizungumza na
kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Kahe waliofikwa na maafa yaliyotokana
na mafuriko.

Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya akizungumza na
wakazi wa kata ya Kahe baada kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika
na mafuriko.

Mbunge
wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho kilicho
fanyika ofisi ya kata ya Kahe, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
Maafa nchini, Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.

Mbunge
wa Viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Lucy Owenya akitoa salamu
za pole kwa wakazi wa kata za Mabogini na Kahe walioathirika na mafuriko
yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


Sehemu ya Msaada uliotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na Mbunge wa jimbola Vunjo, James Mbatia
.

Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Michael Kilawila akikabidhi mfuko wa
Unga kwa baadhi ya wazee katika kata ya Kahe walioathirika na mafuriko
yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.



0 MAONI YAKO:
Post a Comment