Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa
Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina Lissu Mughwai
katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Christina
Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika
kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07
Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam,
alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiaga mwili wa marehemu Christina Lissu
Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chadema katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria Tundu Lissu (Mb)
kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7
mwaka huu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment