April 28, 2016

cpwaa2

 Rapper Cpwaa amesema ukimya wake haumaanishi kuwa ameacha muziki.
Ameiambia Bongo5 kuwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni amekuwa akifanya shughuli zake binafsi zinazohusiana na fani ya IT aliyoisomea.
Amedai kuwa katika kipindi hicho pia amekuwa akirekodi nyimbo kibao huku sasa akijiandaa kufanya video na muongozaji wa ndani.
“Siwezi kurudi kwa style ile ile ya kizamani au kwa strategy zile zile, game imebadilika sasa hivi, watu wako vizuri, wanafanya kazi nzuri,” amesema.
“Nipo kwenye hatua pia ya kuweza kurudi kwenye style ambayo itaweza kwendana na ushindani ambao upo kwa sasa,” ameongeza.
Rapper huyo amesema mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza karibu kila siku kwenye mitandao ya kijamii na sehemu zingine kuhusu ukimya wake na amekiri hilo kumsumbua.
“Ni kitu ambacho kinanikwaza sana, nakaa na watu kwenye mamall nikitoka wanauliza ‘bana vipi mbona umeacha, hebu rudi.’ Challenge ambayo nakutana nayo sasa hivi najiuliza kwenye video labda nifanye na nani. Siwezi kudanganya, siko tayari kutumia $40,000 sasa hivi niende South Africa kufanya video wakati nina majukumu mengi. Kwahiyo siwezi kuchukua hela yangu inayoniingizia mkate wangu wa kila siku kuipeleka huko,” amesisitiza.
“Lakini I promise the industry mpaka kwamba by June watakuwa tayari wameshapata mzigo wangu mpya kabisa.”

Related Posts:

  • TASWIRA YA SHOW YA DIAMOND ALL STAR ELIZABETH NEW JERSEY JITIRIRISHE  All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika.  … Read More
  • RAY C ALITAMANI PENZI LA KIKONGWE MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60. Akizungumza kat… Read More
  • MAJAMBAZI YAUA ARUSHA Mwananchi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi eneo na Clock Tower jijini Arusha. Majambazi hao walikuwa wakipora kwenye Bureau De Change iitwayo Nothern ambapo mareh… Read More
  • ALICHOKIANDIKA WAKILI ABERT MSANDO KUHUSU MSIBA WA ZITTO KABWE   Msando Alberto 7 hrs · Sandown, South Africa · To my brother and friend Zitto Kabwe, I cannot imagine the pain you are going through. All I can say is pole sana for Mama's loss. I pray so that Allah give… Read More
  • MKUTANO YANGA MAMBO SAFIIII Mwenyekiti wa Yanga SC - Yusuf Manji akiongea na wanachama wa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Poilisi - Oysterbay Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE