May 20, 2016

Ali Kiba atakuwa msanii wa kwanza kuonekana kwenye hili jarida maarufu kwa mastaa Duniani.
Ripoti kadhaa zinaendelea kusanukiwa kutoka Johanesburg South Africa, ambapo star wa Bongo Flava anaendelea kutangaza dili 7 kubwa ambazo atazitaja ndani ya saa hizi 48.
Tayari mkali huyu wa Aje amesaini kusimamiwa na kampuni ya muziki ya Sony, ambapo mkataba wa aina yake ni kama aliosaini star wa Nigeria Davido.
Taarifa nyingine ni kwamba Ali ataonekana kwenye jarida maarufu la mastaa Duniani The source ambalo linaheshima kubwa Marekani na atakuwa msanii wa kwanza wa Afrika kuandikwa humo.
Alikiba anakuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kusaini mkataba na Sony World wide, ni mkataba wa miaka mitano, habari yake sio ndogo na sasa atatokea ameandikwa na Jarida maarufu la habari za mastaa Marekani The Source Magazine’
‘Atakua msanii wa kwanza wa Afrika kuandikwa ndani ya hili jarida na hii itamsaidia kujulikana zaidi sababu ni jarida linaloaminika na linalosomwa na mamilioni ambapo kichwa cha habari kitasomeka kuanzia ukurasa wa mbele wa jarida hili’  amesema meneja wake Bi Seven Mosha


Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE