Msanii
Bob Junior amefunguka juu ya kitendo chake cha kuwatoa kimuziki wasanii
Diamond Platnumz na Nyauloso, ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye
muziki.
Akiongea
kwenye PlanetBongo ya East Africa Radio, Bob Junior amesema aliamua
kuwasaidia kwa kuwa aliona ni wasanii wenye vipaji, na yeye alikuwa na
vifaa na studio, na ujuzi wa kutengeneza beats.
“Kina
Diamond niliwatoa kishkaji tu, unajua niliona wana kipaji,halafu
unakuta mtu ana vifaa na studio, hivyo nikaamua kuwafanyia kazi kishkaji
kabisa”, alisema Bob Junior.
Pia
Bob Junior amezungumzia ukimya wake wa muda mrefu bila kutoa kazi
yoyote mpaka sasa alipokuja kuachia wimbo wake na Jose Chameleon wa
Uganda, na kusema kuwa alikuwa anajipanga vizuri na kwa sasa watu
watarajie kazi za mfululizo kutoka kwake.
“Sasa
hivi nimerudi kama unavyoona nina ngoma hiyo na Jose Chameleon, hata
hiyo nimeichelewesha kumpisha Barnaba Clasic baada ya kuona naye
anaachia ngoma na Chameleon, ila kwa sasa watu wajiandae kila baada ya
miezi mitatu nitakuwa naachia ngoma mpya”, alisema Bob Junior.
eatv.tv
0 MAONI YAKO:
Post a Comment