Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema
amesema kitendo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kumng'oa Waziri wa
Mambo ya Ndani Charles Kitwanga kunatokana na Bunge kukosa hadhi
kutokana na mambo ambayo huendelea ndani ya ukumbi huo wa Bunge.
Lema
ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ameyasema
hayo wakati akizungumza na EATV hususu tuhuma za wabunge kunywa pombe
wakati wa kazi.
''Bunge maalumu la katiba Bungeni kulikuwa na 'bar' zinauza pombe na
idadi ya mawaziri na wabunge wanaokunywa pombe haijifichi ni .normal' na
hii inatokana na Bunge kukosa hadhi''
''Hadhi aliyopioteza Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga
imesababihwa na hadhi lililopoteza Bunge na wabunge na viongozi wake,
siku hizi mambo yanafanyika ya ajabu polisi wanaingia ndani ya bunge
wanapiga watu wanachania wanawake nguo, kanuni hazifuatwi, hivyo
Kitwanga katumika tuu kwa namna ya kujiridhisha lakini kupuuzwa kwa
maoni ya kambi ya upinzani ambayo yalieleza kuhusu Waziri Kitwanga
kuhusika na Lugumi ndiko kulipaswa kumng'oa''-Amesema Lema.
Aidha Lema amebainisha kwamba wananchi pia wanapaswa kulumiwa kwa
kitendo cha kuwachagua wabunge na kuwaacha tuu bila kuwafuatilia
wanachokifanya Bungeni.
Kuhusu Bunge kutorushwa 'Live' Lema amesema kwamba inashangaza
kuwaona wananchi wanakaa kimnya, viongozi wa dini na taasisi mbalimbali
na kuwaachia upinzani pekee hali ambayo si nzuri kwa maendeleo ya taifa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment