Hali sasa imewageukia wanawake wenye makalio makubwa kwa kubandikwa jina la chura. Inaelezwa kuwa wimbo huo uliwalenga wanawake wenye makalio makubwa lakini kwavile haukuwa na maadili ukafungiwa. Mitaani sasa Mwanamke yeyote atakayeonekana kuwa na makalio makubwa anaitwa chura, huku akishindikizwa kuwa miluzi na kelele za kila namna kitu ambacho wao wameeleza kuwa usumbufu kwake.
Kufatia wadada hao kukerwa na kitendo hicho na kudai kuwa ni udhalilishaji na kinawanyima raha wanapokuwa maeneo yenye watu wengi, Mkoa wa Kipolisi wa Ilala umepiga marufuku wanaume kuwaita wanawake wenye makalio makubwa “Chura”. Kamanda wa Polisi toka Ilala alisema kuwa mwanamke yeyote atakayeitwa jina hilo atoe taarifa kituo cha polisi na sheria zitachukua mkondo wake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment