May 22, 2016

image 

Manchester United wanatarajia kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya, BBC Sport imeripoti.
Inaaminika kuwa deal hiyo na raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 ilikubaliwa kabla ya ushindi wa United kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.
Ikiwa United imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya chini ya kocha wake wa sasa, Louis van Gaal, uongozi wa Old Trafford unafikiriwa kuamua kufanya mabadiliko yanayohitajika.
Mourinho amekuwa benchi tangu atimuliwe na Chelsea December mwaka jana.
Klabu hiyo imepanga kutangaza ujio wake mapema wiki ijayo baada ya kumwambia Van Gaal, 64, afungashe virago vyake.
Kocha huyo raia wa Uholanzi bado ana msimu mmoja kwenye mkataba wake wa miaka mitatu na licha ya kutumia paundi milioni 250 kusajili wachezaji wapya, ukocha wake umewaangusha mashabiki wengi kwa timu yake kumaliza katika nafasi ya nne na kisha ya tano kwenye ligi kuu ya England katika misimu miwili aliyoifundisha.
Mourinho alikuwa kwenye mchezo wa masumbwi Jumamosi hii ambapo bondia David Haye alishinda lakini alikataa kuongea chochote iwapo anaenda kumrithi Van Gaal.
Mourinho ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi huku akishinda vikombe vitatu akiwa na Chelsea, pamoja na kuingoza  Porto na Inter Milan kwenye ushindi wa ligi ya mabingwa mwaka 2004 na 2010.
Aliwahi pia kuwa kocha wa Real Madrid na kuiwezesha kushinda kombe la Spanish La Liga mwaka 2012.

Related Posts:

  • Brand New Audio | Nipe Tamu - Every Day    Mwanamuziki chipukizi kabisa kutoka mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina la Every Day, amekuletea bonge ya wimbo wake unaoitwa Nipe Tamu. Wimbo umefanywa na Producer Sniper katika studio za Tushi Recordz za… Read More
  • Nahreel kamkatalia Mkenya Producer maarufu wa Tanzania kwenye muziki wa bongoflevaNahreel ameingia kwenye top stories za leo kwenye Dstv.com baada ya kukataa kumpa beat yake staa mmoja wa hip hop nchini Kenya. Nahreel ambaye mikono yak… Read More
  • Ashtakiwa kwa kusambaza picha whatsapp         Miili ya kwanza ya wanajeshi waliouawa Somalia iliwasili Nairobi Jumatatu Mwanamume mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kusambaza picha alizodai ni za wanajeshi wa Kenya waliouawa … Read More
  • Pitio la Magazeti ya leo jumanne january 19, 2016 Karibu mwana familia wa ubalozini.blogspot.com, Leo hii January 19,2016 siku ya jumanne tunakupa tena fursa ya kupitia magazeti yetu ya leo kama yalivyotufikia na kubeba habari zenye uzito wa juu. … Read More
  • Venus Williams apigwa chini katika tenisiKonta ameorodheshwa nambari 47 duniani Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi la Australian Open mjini Melbourne. Konta, 24, al… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE