Mbunge
wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Mngwali amehoji Bungeni kwa nini serikali
isirudishe mjusi ambaye alichukuliwa mkoani Lindi miaka ya 1900's
katika kijiji cha Tandeguru kata ya Mipingo mkoani Lindi na kupelekwa
ujerumani ambapo amehifadhiwa.
''Mkoa
wa Lindi unaongoza kuwa na rasilimali kubwa tumepiga kelele ya mjusi,
mjusi yupo ujerumani wao wanafaidika na mjusi wetu wapanata dola bilioni
3 kila mwaka sisi hatupati kitu''-Amesema Mbunge Riziki.
Mbunge
huyo amebainisha kwamba kama mabaki ya mjusi huyo yangerejeshwa kwa
kuwa ni kivutio kwa ukubwa wake angeweza kuhifadhiwa kwenye makumbusho
nakusaidia ujenzi wa barabara na shule.
Aidha
Mbunge huyo amemtaka waziri wa maliasili na utalii aeleze kwa nini tozo
inayopatikana huko ujerumani haiwafaidishi wananchi wa eneo husika.
Hata
hivyo mjusi huyo mara kadhaa amekuwa akiuliziwa bungeni na serikali
kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kwa manufaa ya wananchi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment