Rapper Kimbunga Mchawi amesema kuwa Nay wa Mitego hajui muziki na wala hajui nguzo za hip hop.
Kimbunga amesema hayo alipohojiwa na kwenye kipindi cha Enews kinachorushwa na East Africa Television.
“Msanii Nay wa Mitego sio msanii mkali, hajui nguzo za hip hop, hajui muziki hata aimbe wimbo gani hawezi, na siwezi kumshirikisha na sijawahi kushirikiana naye, yeye ndo aliwahi kunishirikisha kwenye nyimbo zake, na kwasababu kulikuwa na wasanii wengine kama kina Baghdad, nikaona kazi nzuri nami nikakubali”, alisema Kimbunga.
Wasanii hao wawili wamekuwa na bifu kwa miaka kadhaa sasa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment